TAM YATAHADHARISHA MVUA KUNYESHA SIKU 10 BAADHI YA MIKOA
Tarehe: 12 Oct, 2026
Wakati baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa, Magharibi na Pwani yakitarajiwa kupata mvua zinazoambatana na ngurumo za radi kwa siku 10 kuanzia jana Jumapili Oktoba 11 hadi 20, 2026, maeneo mengine yanatarajiwa kuwa makavu.
Kwa mujibu wa utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) uliotolewa Oktoba 11, 2026, mvua hizo zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Magharibi na Pwani.
Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara ni miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi.
Katika Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, unaojumuisha Tanga, maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, mvua zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, huku Lindi na Mtwara zikitarajiwa kupata mvua nyepesi katika baadhi ya maeneo.
Hata hivyo, utabiri huo unaonesha mikoa ya Dodoma na Singida, pamoja na Nyanda za Juu Kusini-Magharibi zinazojumuisha Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa, inatarajiwa kuwa na hali ya ukavu. Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi.