VINICIUS JR AACHIKA BAADA YA KUBADILI MUONEKANO WAKE
Tarehe: 12 Oct, 2026
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid, Vinícius Júnior maarufu kama Vini Jr., na mwanamitandao maarufu wa Brazil, Virginia Fonseca, wametangaza kuvunjika kwa uhusiano wao wa kimapenzi kwa mara nyingine.
Taarifa hiyo imethibitishwa Jumapili, Oktoba 11, 2026, kupitia ofisi ya mahusiano ya umma ya Virginia Fonseca, ambayo imeeleza kuwa wawili hao hawapo tena kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Katika taarifa hiyo, ofisi ya Virginia ilisisitiza kuwa kutengana kwao hakukutokana na ugomvi wala mgogoro wowote, bali ni uamuzi walioufikia kwa maelewano.
“Virginia Fonseca na Vini Jr. hawapo tena kwenye mahusiano. Hakukuwa na mgogoro wala ugomvi; walifikia tu uamuzi huo kwa maelewano,” ilieleza taarifa hiyo.
Uhusiano wa wawili hao umekuwa na misukosuko kadhaa tangu walipoanza kuwa karibu mwaka 2025. Mnamo Mei 2026, walitengana kwa mara ya kwanza, kabla ya kurudiana Julai mwaka huo.
Baada ya kurejeana, wawili hao waliendelea na uhusiano wao kwa takribani miezi minne. Hali hiyo ilionekana kuashiria kuwa walikuwa wameimarisha mahusiano yao, hasa baada ya kuripotiwa kubadilishana pete za uchumba mwezi Septemba 2026.
Hata hivyo, taarifa za kutengana kwao zimeibuka tena, huku kukiwa na madai ya awali kwamba wawili hao walikuwa na mzozo siku ya Ijumaa jijini Madrid, Hispania.
Ofisi ya Virginia Fonseca imekanusha madai hayo, ikisisitiza kuwa kutengana kwao hakukuchochewa na ugomvi wowote na kwamba uamuzi huo ulifikiwa kwa amani.
Kutengana huku kunaashiria sura nyingine katika uhusiano wa wawili hao ambao umekuwa ukivuta hisia za mashabiki na kufuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari, hasa kutokana na kurejeana kwao baada ya kutengana hapo awali.