National News

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA BILIONI 73.2 KIGOMA

Tarehe: 08 Sep, 2026


Mwenge wa Uhuru umepokelewa na kuanzia mbio zake Mkoa wa Kigoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, ambapo jumla ya miradi yenye thamani ya Shilingi Bil.73.2 itazinduliwa, kutembelea, kukaguliwa sambamba na kukabidhi Hundi, vifaa na Samani.


Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Km. 937.8 katika Halmashauri Nane za Mkoa ambapo katika miradi itakayofikiwa, mchango wa Serikali na wahisani ni Shilingi. Bil.57.5, wahisani Bil.14.6, Halmashauri Mil. 958.4 huku nguvu ya wananchi ikiwa Mil.100.6.

Aidha, Miradi 20 itawekewa mawe ya msingi, 16 itazinduliwa, 12 itatembelewa na kukaguliwa huku mingine minne itahusisha kukabidhi vifaa, Hundi au Samani. Mkoani hapa, Mwenge utakimbizwa kuanzia leo Septemba 7 hadi 14, 2026 kisha kukabidhiwa katika Mkoa wa Tabora Septemba 15, 2026.