Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:
Hamis Abdallah Mkunga ameteuliwa kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Bw. Mkunga anachukua nafasi ya Bw. Mick Kiliba ambaye amemaliza muda wake;
Prof. Alfred Said Sife ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Prof. Sife anachukua nafasi ya Prof. William Anangisye ambaye amemaliza muda wake;
Prof. Alfred Said Sife ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Prof. Sife anachukua nafasi ya Prof. William Anangisye ambaye amemaliza muda wake;
Jaji Mstaafu Wilfred Peter Dyansobera ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA). Jaji Mstaafu Dyansobera anachukua nafasi ya Bw. Edriss Mavura ambaye amemaliza muda wake;
Mhandisi Abdallah Mohamed Mkufunzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha pili;
Dkt. Henry Bethuel Mwanyika ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA. Dkt. Mwanyika anachukua nafasi ya Prof. Leonard Mselle ambaye amemaliza muda wake; na
Prof. John Modestus Lupala ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.