RC SIRRO AWASILI TABORA KUZINDUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MAGHARIBI
Tarehe: 01 Aug, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, amewasili katika Viwanja vya Ipuli, mkoani Tabora, kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi 2026, yanayozinduliwa leo, Agosti 1, 2026.
Maonesho hayo yanayowakutanisha wadau wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na biashara kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Magharibi, yanatarajiwa kutoa fursa ya kuonesha teknolojia za kisasa, kubadilishana uzoefu na kuhamasisha uzalishaji wenye tija kwa maendeleo ya uchumi wa wananchi.