FIFA YAFUTA MPANGO WA KUUZA UMILIKI WA KOMBE LA DUNIA
Tarehe: 01 Aug, 2026
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limefuta rasmi mpango wake wa kuuza hisa kwa wawekezaji binafsi katika mashindano ya Kombe la Dunia, baada ya mpango huo kukumbana na maoni tofauti kutoka kwa wadau wa mchezo huo.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali, ambapo ilibainika kuwa pendekezo hilo limezua mgawanyiko na halilingani tena na malengo yaliyokuwa yamekusudiwa.
Infantino amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kutafuta njia mbadala za kuimarisha maendeleo ya soka duniani huku ikilinda maslahi ya mashindano ya Kombe la Dunia na wadau wake.