Zuchu Athibitisha Ni Mjamzito, Awashirikisha Mashabiki kupitia Instagram
Tarehe: 30 Jul, 2026
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, ameweka wazi kuwa anatarajia kupata mtoto baada ya kushiriki picha inayoonesha ujauzito wake kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Kupitia chapisho hilo, Zuchu amewafahamisha mashabiki wake kuhusu hatua hiyo mpya katika maisha yake, taarifa ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikizua mijadala na kusubiriwa kwa hamu na wengi.
Mara baada ya chapisho hilo, mashabiki, wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa muziki walimiminika kwenye ukurasa wake wakimtumia pongezi na salamu za heri, wakimtakia afya njema katika kipindi cha ujauzito wake.
Tangazo hilo limeibua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakieleza furaha yao na kumtakia kila la kheri Zuchu katika safari yake ya kuwa mama.