TUZO ZA TFF MSIMU WA 2025/2026 KUTOLEWA DISEMBA 2026
Tarehe: 30 Jul, 2026
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema Tuzo za TFF kwa msimu wa 2025-2026, zitatolewa kati ya Desemba 2026, au Januari 2027.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Karia amesema maandalizi ya Tuzo za TFF yameanza kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali, licha ya msimu wa 2024-2025, kutofanyika kutokana na changamo mbalimbali.
"Msimu wa 2024-2025, Tuzo
hazijafanyika kwa sababu ya changamoto mbalimbali ambazo nimezizungumzia mara kwa mara, ila za msimu wa 2025-2026, tunatarajia kuzifanya kati ya Desemba 2025, au Januari 2026," amesema Karia.
Aidha, Karia amesema FIFA na CAF wana utaratibu wao wa kutoa Tuzo, japo kwa Watanzania wamekuwa na haraka ya kutaka mambo bila ya kujua mchakato unaoendelea ndani kwa ndani.
"Unakuta tayari mfungaji bora na kipa bora ameshajulikana kwa sababu wao ni rahisi kujua kutokana vigezo vyao vinavyotumika, lakini kwa wengine kunahitaji mchakato unaohitaji muda," amesema Karia.