Sports

ZIDANE KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA UFARANSA

Tarehe: 28 Jul, 2026


Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) limemtangaza rasmi Zinedine Zidane kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka minne utakaomuweka madarakani hadi Juni 2030, akichukua nafasi ya Didier Deschamps.

Zidane, ambaye aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, anarejea kwenye ukocha baada ya kusimama kwa takriban miaka mitano tangu alipoondoka Real Madrid mwezi Mei 2021.

Katika vipindi vyake viwili vya kuinoa Real Madrid, Zidane alipata mafanikio makubwa, yakiwemo kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, jambo lililomjengea sifa kama mmoja wa makocha bora katika historia ya klabu hiyo. Sasa anatarajiwa kuiongoza Ufaransa katika kampeni za mashindano makubwa ya kimataifa hadi mwaka 2030.