PAMBANENI HADI MPATE KATIBA MPYA - Balozi DKT. NCHIMBI
Tarehe: 24 Jul, 2026
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewahimiza Watanzania kuendelea kuonyesha dhamira na kuongeza juhudi katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, akisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ina nia ya kuendeleza ajenda hiyo.
Akizungumza leo Julai 24, 2026, akiwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Dkt. Nchimbi amesema mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai pamoja na Tume ya Jaji Chande yameonesha umuhimu wa kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya ili kuimarisha utawala bora na demokrasia.
Amesema Watanzania hawapaswi kulegeza juhudi za kudai Katiba mpya, akisisitiza kuwa kuendelea kuipa kipaumbele ajenda hiyo kutasaidia kuhakikisha mchakato unakamilika chini ya uongozi wenye utayari wa kuutekeleza.