WAAMUZI WA TANZANIA WAPEWA MAFUNZO MATUMIZI YA VAR
Tarehe: 23 Jul, 2026
Waamuzi wa mpira wa miguu nchini Tanzania wanaendelea na mafunzo ya awamu ya tano ya matumizi ya teknolojia ya Video ya Kumsaidia Refa (VIKURE au VAR).
Mafunzo hayo yanafanyika katika Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam, yakiongozwa na mkufunzi wa FIFA, Noumandiez Doue, kwa lengo la kuboresha usahihi wa maamuzi na kuongeza uwazi katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Awamu hiyo ya tano (Moduli ya Tano) inafanyika kuanzia Julai 21 hadi 26, 2026, huku sehemu kubwa ya mafunzo ikihusisha mazoezi ya vitendo uwanjani ili kuwawezesha waamuzi kutumia kwa usahihi vifaa na teknolojia ya VIKURE.