Breaking News

KLABU YA SIMBA YAPATA PIGO KIFO CHA KIONGOZI WAKE

Tarehe: 23 Jul, 2026


Klabu ya Simba imepata pigo baada ya mwanachama na kiongozi wake Idd Kajuna kufariki dunia baada ya kuugua kwa siku saba. Kajuna amefariki leo Alhamisi, Julai 23, 2026 alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Hadi anafariki Kajuna alikuwa mjumbe wa kamati ya mashindano ya Simba, ambapo pia amewahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya timu hiyo. 

Simba imethibitisha kifo hicho cha Kajuna huku ikitaarifu kuwa atazikwa leo katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. 

“Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa tarifa ya kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Iddi Kajuna kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.