#MICHEZO: Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kumsajili mlinzi wa pembeni Nathan Chilambo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa mashindano wa 2026/27.
Chilambo ni mchezaji anayemudu kucheza nafasi za beki wa kulia na beki wa kushoto, jambo linalompa uwezo wa kuongeza chaguo katika safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi.
Usajili huo ni sehemu ya maboresho yanayoendelea kufanywa na Simba SC katika kujiandaa na mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao.
Sikiliza MAIN FM kupitia 91.7 Mhz Kigoma, Kasulu, Uvinza, Buhigwe.
Pia tufuatilie kwenye Mitandao ya Kijami, Instagram, Facebook, TikTok, na Youtube Main FM Tanzania pia tusikilize kupitia www.mainfm.co.tz pia Radio Box na Radio Garden tafuta Main FM
Fuatilia Youtube Chaneli Yetu ya Main FM Tanzania.