National News

MADAKTARI WASIO NA MIPAKA WASAIDIA VIFAA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU KASULU

Tarehe: 29 Sep, 2025


#KIGOMA:Shirika la Madaktari wasio na mipaka (MSF) limetoa msaada wa vifaa Vya matibabu pamoja na kutuma watalaamu wake kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya mji wa Kasulu Mkoani Kigoma.

Shirika hilo la madaktari wasio na mipaka la (MSF) limetoa pia msaada wa vifaa vya matibabu pamoja na kumtuma mtaalamu mbobezi wa mambo ya Mazingira kutoka makao makuu Dar es salaam ili kusaidiana na wataalamu wa afya wa halmshauri ya mji wa Kasulu katika kituo maalumu cha kutolea huduma za wagonjwa wa kipindupindu katika kata ya Nyansha ili kubaini njia bora za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Mwakilishi kutoka shirika la (MSF) Awa Amadu anaeleza kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi halmashauri ya mji wa Kasulu namna watakavyoendelea kushirikiana na halmashauri kudhibiti mlipuko wa kipindupindu.

Mbali na msaada huo wa vifaa hivyo vya matibabu shirika la MSF limetoa mafunzo kwa wataalumu wa afya pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii idadi kwa ujumla 165 kutoka vituo vya Serikali na Binafsi katika wakati ambao bado kunashuhudiwa ongezeko la wagonjwa wakipindundu na kata 9 kati ya kata 15 za halmashauri ya mji wa kasulu zikiwa tayari zimeripoti kesi kadhaa za ugonjwa huo ambapo hapa Mratibu wa huduma za afya na matibabu kwa jamii halmashauri ya kasulu mji Dkt kazimoto sangwa anasisitiza jamii kuendelea kuchukua tahadhari.

Hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa hasa katika taasisi za Elimu ikiwa ni kuhakikisha mafanikio yanapatikana katika kudhibiti kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu kama anavyoeleza Mratibu wa afya shuleni na mratibu wa usalama wa chakula kwenye jamii Kasulu mji Bw.Gilbert Moshi.